KUONDOA WEUSI MAKWAPANI


Leo napenda kuongelea kuhusu usafi wa makwapani.Watu wengi wanapenda kujua ni jinsi gani wataweza kutoa weusi wa makwapani maana limekuwa ni tatizo la wengi kwa wanaume na wanawake.Hii njia ni rahisi na salama kila mutu anaweza kujaribu akiwa nyumbani.

Mahitaji
  1. Baking soda
Baking soda ndo hiyo yenye rangi nyekundu na blue(bicarbonate of soda) zinapatikana madukani kote.










Kuna nyingne unaweza kuzipata hata supermarket







2. Mafuta ya nazi
Mafuta ya nazi watu wengi wanajua jinsi ya kutengeneza ila ntawaletea nakala jinsi ya kutengeneza mafuta ya nazi kwa wasiojua kutengeneza.Ni vizur ukatumia mafuta ya nazi yale yenyewe ambayo hayajachanganywa na kitu kingine chochote








JINSI YA KUANDAA
  • Weka baking soda ya kutosha na mafuta ya nazi katika bakuli lako











  • Koroga vizuri kutengeneza mchanganyiko usiwe mwepesi wala mzito
  • Pakaa mchanganyiko wako makwapani na sugua taratibu kwa dakika chache.Acha kwa muda wa dakika 5 had 10 na nawa vizuri. Ni vizuri kuoga moja kwa moja. Jifute vizuri na taulo au kitambaa kisafi
            
  • Fanya zoezi ili kwa wiki mara 3 au mbili kutegemea na tatizo lako.Unaweza kufanya kwa wiki mara moja au kwa wiki mara 2 au 3 kwa jinsi utavyopendelea mpaka utakapopata matokeo mazuri.
Mchanganyiko huu wa baking soda na mafuta ya nazi pia unaweza kuutumia usoni pia.
Baking soda ina matumiza mengi tutaangalia matumizi yake taratibu,baking soda inatumika pia katika kutakatisha meno na kuwa meupe,kuondoa madoa na chunusi usoni bila kusahau baking soda pia unaweza kuituma katika usafi wa majumbani mfano katika kusafisha choo..Hivi vyote nitawaletea ili wote tuweze kujifunza urembo na usafi kwa njia za asili..
Mafuta ya nazi aisee yanafaida nyingi sanaaa ambazo taratibu kila siku nitaweza kuwajuza.ASANTE

Comments

Popular Posts